Msinifananishe Na Huyo Mla Unga.


Msanii wa Hip Hop nchini Dogo Janja aliyekaa kimya juu ya kauli za Young Killer na Young Dee, sasa kafunguka na kusema Young Killer alimwambia hamuwezi ni kwa sababu alishakuwa role model wake, lakini alisema hakupenda Young Dee kumuita yeye ni kifaranga.
Alipoulizwa juu ya kauli ya Young Dee kumuita kifaranga, alifunguka: “Mimi pia sipendi kufananishwa na kifaranga japo sijakataa kufananishwa na Young Killer kwa sababu alishawahi kuwa role model wangu, kwa hiyo kufananishwa naye si kitu kibaya, lakini kufananishwa na mla unga Young Dee ndiyo sipendi tena mnakosea kabisa.
“Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani tuzungumze lakini kufananishwa naye sasa hivi sitaki kwani ni mtu ambaye ukimuacha nyumbani kwako unawaza vitu vyako kama TV, radio na vingine. Je, utavikuta salama, maana asije kuiba kwenda kuuza,” alisema Dogo Janja
Hawa ni vijana wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Hip Hop nchini, ambako pia watu wanawafananisha kutokana na wote wanavyoimba kwa aina ya kurap ila kwa kila mmoja hapendi kufananishwa na mwenziye

Source: Udaku.