Staa wa Filamu ya Home Alone amefariki

Home Alone ni moja ya Filamu ambazo zilikuwa zinafanya vizuri sana Duniani ambapo ilijizolea umaarufu mkubwa Tanzania lakini habari mbaya kuhusu Filamu hiyo ni kifo cha mmoja wa waigizaji wake John Heard akiwa katika Hotel Ijumaa.

John Heard ambaye amefariki akiwa na umri miaka 72 alikutwa amefariki na mhudumu wa Hotel mjini California Ijumaa, kwa mujibu wa taarifa ya familia.

Katika mfululizo wa filamu ya Home Alone, John Heard aliigiza kama baba wa Macaulay Culkin ‘Kevin’ lakini mbali na filamu hiyo aliigiza pia Big with Tom Hanks, Gladiator na The Pelican Brief, wakati katika kazi za TV alishiriki katika Battlestar Galactica na The Sopranos.

Source: Millard ayo