Nick wa Pili awashauri waongozaji wa Video.

Mwana hip hop kutoka Weusi Company, Nick wa Pili amesema ili waongozaji wa video za muziki hapa nchini waweze kufanikiwa, ni lazima waepuke kuigana.

Madirector wa Bongo wanachangamoto ya video kufanana, idea kufanana au aina ya vitu ambavyo vinakuwa kwenye video kufanana.”

“Mimi nafikiri uwanja wa video ni mpana sana, nafikiri suala la imagination kiwe kitu kikubwa kwao yaani ukiamua kuimagine hautashindwa kitu chochote. So nawaomba madirector wajaribu kuimagine, wajaribu kufanya kitu ambacho mtu mwingine hajakifanya au yeye hajawahi kukifanya zamani, yaani mpaka rangi za video zinafanana hii kitu sio nzuri kabisa na inawashusha viwango.

Source: Dizzim online