Msanii Future Wa Marekani Adata

Rapa kutoka Marekani, Future amesema Hip Hop inayofanywa na Wasanii wa Afrika ni nzuri kwani inawavutia wasanii wengi wakubwa wa Marekani kuisikiliza.

Future amesema Hip Hop ya Afrika inaelezea uhalisia wa Mazingira ina’sound nzuri pia hata midundo yake inavutia kuisikiliza.

“Hip Hop ya Afrika inasound vizuri sana inavutia kuisikiliza kwani imejaa ubunifu na huwa naingia studio kusikiliza midundo yake kuona kama ninaweza kufanya kitu“,amesema Future.

Hata hivyo, Rapa Future baada ya kunogewa na midundo ya kiafrika amethibitisha kuwa tayari amefanya kolabo na WizKid kutoka Nigeria .

Source: Udaku