Shilawadu Wajuta Kwenda Kwa King Kiba.

Imebainika kuwa licha ya vijana hawa wa shilawadu kuwa na kipaji cha kunyapia umbea, wanakipaji kingine cha ziada cha kukimbia mbio fupi na hata zile ndefu kwa kasi kubwa zaidi hata kumshinda Usain Bolt.

Hayo yamebainika baada ya vijana hao kunyapia umbea nyumbani kwa Alikiba mda wa usiku na kukutana na bonge la mbwa jike aitwae rubi ambae hata hakuwabwekea lakini kutokana na uzoefu na kumbukumbu za hivi karibuni za kuingiliwa katika eneo lao la kazi na machine gun za kisasa waliamua kufunga turbo kwenye miguu yao na kukimbia mbio mithili ya mashindano ya olympic hali iliyopelekea kukosa umbea uliowapeleka kwa King Kiba, mzee wa Aje anayemiliki BMWX5 la kisasa kabisa…
Source: Udaku