AliKiba kuvunja ukimya.

Staa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na Mkurugenzi wa kampuni ya RockStar4000 AliKiba amewaweka tayari mashabiki wa muziki wake na Bongo Fleva kwa ujumla kuwa leo anachia ngoma yake mpya ilioonekana kuwa moja kwa moja kuwa itakwenda kwa jina ‘SEDUCE ‘jina lenye maana ya ushawishi wa kimapenzi’ ama kupeipeti katika tafsiri halisi ya lugha ya Kiswahili.

Kiba ambaye amekuwa kimya kwa muda kiasi cha baadhi ya mashabiki kusubiri huku wasiache kumtupia lawama kwa kukaa kwake kimya kwa kipindi kirefu ambapo wimbo huu utakuwa ni wimbo wa kwanza wenye wazo la pekee kwa AliKiba kuuachia kwa mwaka wa 2017 ukiacha na Aje Remix iliyoachiwa rasmi mwazo mwa mwaka huu ambayo toleo la awali la wimbo huo liliotoka Mei, 2016.

Hata hivyo kukaa kimya kwa muda mrefu katika utaratibu  wa AliKiba wa kuachia nyimbo limekuwa ni jambo ambalo mashabiki kwa sasa wanalipiga vita kutokana na idadi kubwa ya mashabiki kutaka kusikia kazi nzuri kutoka kwake ili kukata kiu yao na kufurahia kazi nzuri kutoka kwa msanii wao wanaompenda.

Source: Dizzim Online.