Mwanamke Anayelipwa Zaidi HollyWood.

Emma Stone ndiye muigizaji wa kike wa Hollywood anayelipwa mkwanja mrefu zaidi, kwa mujibu wa Forbes. Mwaka jana pekee, mrembo huyo ameingiza dola milioni 26. Amempiku Jennifer Lawrence aliyekuwa akiongoza orodha hiyo na kumtupa hadi nafasi ya 3 kwa kuingiza dola milioni 24.

Jennifer Aniston amekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 25.5, Melissa McCarthy, aliyekuwa nafasi ya pili mwaka jana amekamata nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 18 na Mila Kunis kukamata nafasi ya tano.

Source: Dizzim online