Latifa Mohamed aka Queen Tipha amefunguka baada ya kusambaa mitandaoni picha za mzazi mwenzake, Ben Pol akionekana wakibusiana na Snura wakati walipokuwa mkoani Tabora kwa ajili ya tamasha la Fiesta.
Queen Tipha amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa hakushtuka baada ya kuona picha hizo kwa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa kazini.
“Nimeamka asubuhi nikaona watu wengi wamenitag, nilichukulia kawaida kwa sababu ni mtu ambaye ninamuamini na aliniaga kuwa anaenda kazini,” amesema Queen Tipha.
“Sikuona kama ni kitu cha ajabu kwa kuwa yule ni msanii mwenzake na rafiki yake pia. Nimechukulia kawaida tofauti na watu wanavyofikiria,” ameongeza. Queen Tipha aliwahi kuwa mshindi wa pili kwenye Miss Tanzania 2013 na wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja na mpenzi wake Ben Pol.
Story By:@Joplus_
Source: Udaku Special Blog