Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa’- Rais Magufuli

Wakati Tanzania ikiomboleza vifo vya watu 32 wakiwemo wanafunzi 29 waliopata ajali ya gari mkoani Arusha May 6, 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kupitia ukurasa wake wa twitter kayaandika haya kuhusu msiba huo.

‘Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha 1/2’- Rais Magufuli

‘Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania‘- Rais Magufuli

Source: Millard ayo