Jux akanusha tetesi za kuachana na Vanessa Mdee, adai wameamua kutoonesha uhusiano wao tu


Siku za hivi karibuni zimeibuka tetesi kuwa Penzi la Jux na Vanessa Mdee limevunjika, Jux amejibu tetesi hizo.

Kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jux amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa Ilifika kipindi mashabiki walikua hawaongelei kazi zao zaidi ya mapenzi tu hivyo wakakubaliana kutoonesha uhusiano wao ili mashabiki wafocus na kazi zao.

Aidha Jux amesema tetesi hizo ambazo ziliibuka kuwa alishindwa kwasababu ya wivu baada ya picha za Vanessa Mdee na Ice Prince wakishoot video kusambaa mtandaon, Jux amesema anamsupport mpenzi wake huyo kwasababu alikuwa kazini.

Source: Teamtz