Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang ametemwa

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang ametemwa katika kikosi cha timu hiyo kutokana na maswala ya ukosefu wa nidhamu.

Ripoti kutoka Ujerumani zinasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alichelewa katika mazoezi lakini Aubemayang anasema kuwa alikasirishwa na uamuzi huo.

Aubameyang hatashirikishwa katika mechi dhidi ya VFB Stuttgart siku ya Ijumaa.

Dortmund ilitangaza kumsimamisha kwa muda mchezaji huyo ikijibu maswali ya mashabiki wake katika Twitter, lakini haikuelezea sababu ya hatua hiyo.

Raia huyo wa Gabon pia alisimamishwa kwa muda mwaka uliopita baada ya kuelekea Italy bila ruhusa ya klabu hiyo.

”Sielewi ni kwa nini, nilizuiwa kuelekea Milan kwa sababu siku heshimu sheria , lakini wakati huu nimekasirishwa sana , sikutaka kuwasili nikiwa nimechelewa”, aliambia gazeti la Bild nchini Ujerumani.

Dortmund imepoteza pointi tatu katika mechi zake nne na hivyo basi kushuka katika jedwali la ligi pointi sita

@moodyhamza