Makali ya Weusi yamfika shingoni Pink

                                     

Rapa wa kike chini ya lebo ya muziki ya Syle Record kutoka Tanzania anayefanya vyema na wimbo wake ‘Unafeel Aje ’ Pink amezidiwa na hisia zenye shahuku ya kutaka kufanya kazi na kundi la wasanii wa muziki wa rap anaowakubali kutoka Tanzania.

Amesema kuwa, kwa Tanzania ameshabahatika kufanya kazi na wasanii wakubwa ambao ni Young D na Mr. Blue wasanii ambao hawajakata kiu yake ya kutamani kufanya kazi na Weusi kundi linaloundwa na G-Nako, Joh Makini, Nikki wa Pili na wengine wawili ambao hawaonekani kushiriki sana katika kazi za pamoja kama kundi ambao ni Bonta na Lord Eyez.

“nimesha fanya kazi na Young D, Mr. Blue lakini pia nina hamu ya kufanya na some of the artist kutoka Tanzania kama ikitokea nafasi napenda sana kufanya na Weusi…yeah wanani-inspire a lot kwa hiyo incase ikatokea kwamba kuna kolabo ambayo natakakiwa nifanye napenda sana kufanya na Weusi” Alisema Pink.

Hata hivyo Pink amegusia kiasi kuhusu kutanua wigo wake wa soko la muziki kuwa menejimenti yake ya Style za kimbele iko katika hatua za kumtafuta msanii hasa wa kike anayefaa na mwenye uwezo kutoka nchini Kenya kwa mipango ya kufanya kazi ambayo inatazamiwa kuunganisha Afrika Mashariki na kuweka nguvu zaidi kwa marapa wa kike.

                                                                Source: Dizzimonline