Billnass akaribia kumaliza Shule.

Ukiwa umebeki muda mfupi tu hadi msanii wa hip hop nchini, Billnas ahitimu elimu yake shahada ya kwanza, amezungumzia maisha yake ya baadaye na changamoto alizozipata kwa wakati mzima akiwa chuoni.

Msanii huyo amesema kufanya muziki na shule ni kitu kigumu na kinahitaji umakini zaidi. “Unajua saa zingine unakuta napata show halafu ni time hiyo hiyo ambayo ninakuwa na mitihani, so kwa upande wangu nakuwa na wakati mgumu sana ila kwavile shule ni muhimu inanibidi nifanye mitihani,” amesema rapper huyo ambaye anasomea kozi ya Procurement and Supply management katika chuo cha CBE.

Aidha ameongeza na kusema, “Baada ya kumaliza chuo, sifikirii kuajiriwa, nataka niwe mfanyabiashara ingawa ikitokea ajira nitafanya ili nizidi kuongeza kipato cha biashara nitakayopanga kuifanya kwa wakati huo.”

Hivi karibuni Bill alipewa shavu la kutosha na Mwana FA kwenye ngoma yake Mazoea.

Source: Dizzimonline