Madee amemtaja msanii anayefaa kuwa Rais

Rapa staa wa Bongo Fleva Madee kutoka Manseze ambaye anatamba na wimbo wake wa HELA amebainisha kuwa iwapo itafika siku ambayo ataondoka Manzese, atamrithisha mikoba ya Urais mkali mwingine wa Hip Hop nchini Fid Q.

Akizungumza na mtangazaji wa 255 ya XXL ya Clouds FM, Madee amedai kuwa Fid Q ni msanii mwenye uwezo wa ziada tofauti na muziki anaoufanya kitu ambacho kinamfanya awe tofauti hata wakati wa kuzungumza ukilinganisha na wasanii wengine>>>”Kama itafika siku naondoka Manzese, Urais nitamuachia Fid Q. Ukiachana na muziki, Fid ni zaidi ya msanii.” – Madee.

Source: Millard ayo