Alichokiandika Naibu Waziri Kigwangalla kuhusu perfume ya Diamond

Siku chache baada ya staa mwimbaji Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake mpya “Chibu Perfume” na kuonesha kupokelewa kwa nguvu kubwa nchini Tanzania, Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla ameandika ujumbe kuhusu perfume hiyo huku akimsifia Diamond kwa kufanya vitu vikubwa pamoja na kukiri kuwa yeye sio shabiki wake isipokuwa anaupenda muziki wake.

“Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and businessman.

He does business in music, he does a business of entertainment. Sasa naona kupitia kipaji chake cha ujasiriamali, naona ameamua kuwa muwekezaji, an investor! This is incredible. Keep stepping up your game son, that’s the way to do it! Hakika wewe umetoka #NjeYaBox, na Mungu akuongoze ubaki huko huko juu, usishuke!

I wish wasanii wenzako pia watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara kwenye vipaji vyao, wageuze changamoto kuwa fursa, waache kulalamika, wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa zenu, kwa hakika mtafanikiwa sana!

 Source:Millard ayo