Muandishi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mabeste amedai kuwa hajawahi kuwa na urafiki na wasanii wenzake kwa kuwa hapati mawazo mapya na kufunguka rafiki yake mkubwa ni mke wake.
Mabeste Mke wake na Mtoto wake
Mbele ya kamera za eNEWZ ya EATV, Mabeste amefunguka hayo kwa kusema kuwa wasanii wengi anaonekana nao wanakutana kikazi na siyo kirafiki kwani hawampi mawazo mapya ya kumfanya ajiongeze katika kazi zake.
Msanii huyo ameendelea kufunguka kwamba na tofauti na mke wake marafiki zake wengine ni watu waliopo nje ya muziki kwa kuwa wao ndio wanaona kipi kinafanyika katika tasnia na ndio washauri wa kumuelekeza kipi cha kufanya na kipi cha kuacha
“Ukiacha kuwa kwa wasanii kuna unafki mimi mke wangu ndiyo rafiki yangu. Huwezi kunikuta katika sehemu za starehe kwa sababu sina hao marafiki wa kutoka nao. Mimi na wasanii wenzangu tukikutana ni kwa ajili ya kazi tuu. Unajua mkiwa uwanjani hamuoni mnayoyafanya, ila waliopo nje ndo wanajua. Hata nikisema wasanii wenzangu ndio wa kushauriana nao basi itafika sehemu mawazo yatafika ukomo kwa sababu tunawaza wote sawa. Kitu kingine naweza kusema marafiki wa Mabeste ni wa Mabeste peke wala siyo wa William ndio maana nasema marafiki zangu ni watu wa kawaida siyo ma – star” – Mabeste
Source: Udaku