Njia Sahii ya Kutunza Miguu Yako..!!!

Miguu ni sehemu inayoangaliwa sana hasa kwa wanawake, kwani unapoamua kuvaa nguo fupi na huku miguu yako haiko katika hali ya kuvutia sina shaka utaanza kujishuku hata kabla ya kutoka nje.
Miguu ni sehemu ambayo inatakiwa kutunzwa kwa kipekee kama ilivyo sehemu nyingine kama usowengi tumekuwa tukipendezesha nyuso zetu na kusahau kabisa habari za miguu.
Haijalishi miguu yako ni miembamba au minene iwapo utaitunza vizuri sina shaka kuwa utavutia kwa nguo yoyote utakayoivaa.
Kuna njia nyingi za kutunza miguu na unaweza kutunza miguu yako hata kama huna fedha za kununulia vikorokoro vinavyotakiwa.
Unaweza kuchukua beseni na kuweka maji ya uvuguvugu yenye povu la sabuni maalum ya kuoshea miguu kisha loweka miguu na iache kwenye maji kwa muda wa robo saa hivi.
Chukua aina ya scrub uliyoichagua kwa ajili ya miguu yako paka na ikikauka anza kusugua miguu yako na hadi kwenye vidole na unyayo.
Kisha jisafishe kwa maji ya uvuguvugu.
Baadhi ya vitu unavyoweza kutumia ili ku kutengeneza miguu yako ni pamoja na foot file, Therapysa virgin vie salt scrub, Pedicure iliyotengenezwa kwa OPI Refresh Cooling fot Gel, Innoxa cool na Calm liquid talc na Feet first reviving Foot Soak.
Kwa wale ambao miguu yao ina makovu au madoadoa wajaribu kutumia scrub na kama hawatafanikiwa kuondoa tatizo hilo basi wanashauriwa kutumia cream na sabuni zenye mchanganyiko wa ukwaju kwani zinasaidia sana kuondoa madoa.
Pia unaweza kuchukua mkwaju ukaloweka kwenye maji ukishalainika changanya mchanganyiko huko na asali kasha paka.
Husaidia kuondoa madao na hata kwa wale wenye ngozi za mafuta na chunusi sugu mafuta yatakauka na chunusi hazitatoka tena.