MAMBO 10 Muhimu Ya Kuufanya Uume Kuwa Na Afya

Uume (Penis) ni kiungo chenye hisia na muhimu katika jinsi ya kiume kutokana na nafasi yake katika mwili.
Wanaume wengi wamekuwa wakitumia kiungo hicho pasipo kuzingatia utunzaji wake nakuifanya sehemu hiyo nyeti kuwa chafu na hata pengine kutoa harufu mbaya kwa kutoifanyia usafi sawasawa hasa baada ya kushiriki tendo la ndoa na kusisahidia haja ndogo.
Leo kati safu hii ya afya nikakufahamisha jinsi 10 muhimu za kutunza uume wako:
Usafi kwa asiyefanyiwa Tohara
Watu wengi usahau hata kushindwa kusafisha ngozi ya juu ya Uume wakati wa kuoga na baada ya tendo la ndoa na hasa wale ambao bado wana Ngozi ya juu ya uume (govi) na kusahau kusafisha eneo la chini yake. Kama una ngozi ya mbele katika uume (govi), unapaswa kuvuta kwa chini kwa upole ngozi hiyo na kufua eneo la chini yake na maji moto. Kama utashindwa kufanya hivyo utasababisha eneo hilo kuwa na harufu mbaya na kusababisha kuzaliana kwa bakteria.
Kunawa mikono
Ni lazima kuwa na tabia ya kusafisha uume wako si tu baada ya kutoka chooni lakini pia kabla. Osha mikono yako wakati wowote kabla ya kugusa uume wako. Hii ni kutokana kushika vitu vingi ambapo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kutunza kemikali. Pia ni muhimu kama umekuwa katika kuwasiliana na watu hivyo uweza kubaki na chembechembe ambazo zinaweza kusababisha muwasho kwa kushika pilipili hivyo utajikuna na kusababisha michubuko katika uume.
Uchunguzi wa Mara kwa Mara
Si tu kama wanawake wenyewe ndio wanashauriwa kujitegemea kwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti na kizazi, Lakini pia wanaume wanapaswa kuwa na utaratibu wa kuangalia sehemu zao za siri kama wana uvimbe wowote na pia kwa ishara ya magonjwa ya zinaa. Kuchunguza pia shahawa yako kutambua mabadiliko yoyote katika muonekano au uwepo wa damu katika uume.
Epuka Majeraha
Uume wako unahitaji ulinzi, upendo na huduma kutoka kwako sambamba na kuepuka hali ambazo zinaweza kusababisha majeraha katika uume. Hii inaweza kutokea kwenye ngono isiyo salama au punyeto bila kurainisha ngozi. Pia kuhakikisha unaepuka kuvaa nguo ya ndani (chupi) ambayo haibani sana. Ni vyema ukapata muda wa kukaa bila nguo ya ndani (chupi) ili kuweka wazi uume na kuepusha msuguano utakaoweza kuleta madhara.
Kuwa na mwanamke mmoja
Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja uua uwezo wako kingono lakini pia kuwa na mwanamke mmoja kutakusaidia kuwa mwenye tabia njema na kuwa na nguvu na uwezo mzuri wakati wa kufanya tendo la ndoa na hasa kabisa kujikinga na magonjwa ya zinaa.
Kupata muda wa Mapumziko
Hii ni nzuri kwa afya yako kwa ujumla lakini nzuri hasa kwa uume wako kuwa na afya. Kila wakati kila unapokuwa umepumzika kwa usingizi mzito, uume wako utakuwa na uimara kutokana na kuupumzisha. Hii ni muhimu kwa sababu husaidia kurejesha sura yake na pia kuongeza muda wa utendaji kazi wa damu yenye oksijeni.
Kunywa maji
Kuwa na tabia ya kunywa angalau glasi nane za maji safi. Maji huvuta sumu nje ya mwili wako na kuruhusu damu kufanya kazi na kuongeza kukusisimua wakati wa tendo la ndoa.
Uchaguzi wa sabuni ya Kuogea na mafuta
Ni vizuri na muhimu kufanya usafi wa sehemu za uzazi. Na hata hivyo haipaswi kwenda kuosha na kuskrabu sehemu za siri kwani ngozi ya uume ni raini na nyeti. Matumizi ya sabuni ambazo uondoa vidonda si nzuri kwa kutumia katika uume na kwa kutumia kama njia ya kurainisha uume wakati wa tendo la ndoa lakini pia ni kivutio cha maambukizi. Vizuri kuosha mara mbili kwa siku na maji ya joto kwa kutumia sabuni za kawaida.
Kwa nini unapaswa kunyoa
Mwanaume unaweza kutoona umuhimu wa kunyoa kama ilivyo kwa mwanamke lakini ukweli ni kwamba hata wewe unapaswa kunyoa na kutumia nyia nyepesi za kunyoa ili kuweka eneo lako la uzazi laini na safi. hivyo kama kunyoa mwenyewe kutakuwa na kisingizio mnaweza kufanya hivyo pamoja kama wanandoa hivyo mwenza wako akakuweka katika hali ya usafi.