AT azungumzia kinachoendelea kati yake na Msami

Siku chache zilizopita kulikuwa na taarifa zilizodai kuwepo kwa ugomvi baina ya wasanii wa Bongofleva Msami dhidi ya AT ambapo moja ya iliyotajwa kuwa sababu ni namba ya simu ya Msami kukutwa kwenye simu ya mwanamke aliyekuwa na mahusiano na AT.

Leo April 26, 2017 Ayo TV na millardayo.com imekutana na AT ambaye moja ya mambo aliyoyatolea ufafanuzi ni kuhusu chanzo cha ugomvi baina yake na Msami ambapo alisema:>>>”Ukweli, sababu sio mwanamke. Mwanaume ukigombania mwanamke haileti picha. Siwezi kugombania mwanamke na Msami. Msami anachukua wanawake au anachukuwa watu walioumbwa? Labda yeye anatafuta njia ya kunitafuta. Mwanamke gani nitamgombania na Msami halafu nichukue simu nikute namba yake nianze kupigizana naye kelele? Hakuna kitu kama hicho, sijawahi kabisa.

“Mwanamke ambaye najua alikuwa mshikaji wangu ambaye ni mwanamke wake ni Uwoya. Sasa sijui analizungumzia hilo. Akitaka nimuoneshe ukaribu wangu na Uwoya nitamuonyesha. Uwoya alikuwa shabiki wangu kweli kweli hata nilipokuwa nikikutana naye, nilikuwa namueleza vitu vya msingi. Labda yeye Msami alikuta namba yangu kwenye simu ya mpenzi wake ndio akatafuta chokochoko, lakini sio mimi.” – AT.

Source: Millard ayo