Baada ya kucheza mchezo wa El Clasico dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Real Madrid leo wataingia uwanjani kucheza dhidi ya Deportivo La Coruna katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Hispania.
Real Madrid watacheza mchezo wa leo wakiwa bila mchezaji wao tegemeo Cristiano Ronaldo na Toni Kroos kutokana na kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane kuamua kuwapumzisha wachezaji hao katika mchezo watakaocheza ugenini katika uwanja wa Riazor.
Kwa sasa kufuatia maamuzi hayo ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane, kikosi cha Real Madrid kitawakosa wachezaji wanne Garth Bale anayesumbuliwa na majeruhi na Sergio Ramos aliyeoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa El Clasico.
Source: Millard ayo