Kauli ya Lionel Messi baada ya ushindi vs Real Madrid

Usiku wa April 23 FC Barcelona walikuwa katika uwanja wa wapinzani wao Real Madrid kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi Kuu Hispania, katika mchezo huo FC Barcelona walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Real Madrid.

Magoli ya FC Barcelona yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga magoli mawili na Ivan Rakitic, hivyo kufanikiwa kuondoka na point tatu dhidi ya wapinzani wao wa jadi na kufufua matumaini ya kuwania LaLiga ambalo kama wangepoteza mchezo wa jana wangekuwa katika nafasi finyu zaidi ya kutwaa taji hilo.

Leo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona Lionel Messi ameizungumzia game hiyo “Tulienda Bernabeu kuhakikisha tunapata ushindi na kurudisha nafasi yetu ya kupigania Ubingwa wa LaLiga bado tuna safari ndefu” >>> Lionel Messi

Source: Millard ayo