KWANINI NI VIGUMU KUPUNGUZA UZITO NA UNENE WA MWILI WA BINADAMU?

Napenda kukupongeza ewe msomaji wa makala zangu za afya kama hukusoma hatua ya kwanza tafadhari bofya profile yangu FACEBOOK NAITWA KB MKUMBO OR TEXT/WHATSUPP 0767074124 usome huu ni mwendelezo wa kwa nini hupungui uzito ingawaje unajinyima kula vyakula. Imekuwa ni desturi kwamba watu wengi wenye uzito mkubwa wamekuwa wakitumia taarifa zisizo rasimi ili ziwasaidie kupungua uzito ambavyo sivyo inafikia hatua wanakumbwa na mambo hatari ya kiafya kama yafuatayo:
~Kukosa lishe ya kutosha yani madini na vitamini muhumi vinavyorutubisha mwili na kupigana na magonjwa kwa mfano vitamini c
~Kukosa vyakula vya kujenga mwili na kuimarisha shughuli za mwili kama ubongo kufanya kazi vizuri na vyakula vya kuondoa mafuta mabaya mwilini.
~Kupata magonjwa sugu kama viodonda vya tumbo
Kuongezeka uzito zaidi ya ulivyokuwa na kuwa hatarini kupata magonjwa sugu kama pressure na kisukari nk

ZINGATIA
~Unapotaka kupungua uzito tumia ushauri wa kitaalamu na chakushangaza kuwa tukiongelea kitaalamu mnazani naongelea daktari unaye mkuta ofsini kapiga koti, Bali ni mtumishi wa afya ambaye anafahamu elimu ya lishe kwa undani wake. Kumbuka na inasikitisha hadi sasa watumishi wengi wa afya hawajui kuwashauri wagonjwa kuhusu lishe. Hii ni kutokana na mitaala yetu ya Tanzania daktari au nurse kufundishwa dawa na magonjwa mbalimbali bila kujua nini hasa chimbuko la hizo dalili.

SEHEMU YA PILI: EPUKA VYAKULA VYA SUKARI NYINGI
Ndg msomaji vyakula vya sukari nyingi yani HIGH GLYCEMIC FOODS ni tatizo na changamoto kwani jamiii tayari imesha dhurika na hivyo vyakula. Kwani mtu hawezi kula bila soda pembeni, huo sio ufahari bali bali unakaribisha magonjwa kwani SUKARI ndio kiini cha magonjwa yote humu duniani sugu.
Utumiapo chakula cha sukari nyingi kinasababisha uchovyaji wa insulin kuwa juu kupita kiasi na hatimaye kusababisha vichocheo vya mwili kama estrogen kwa wanawake kutosawazika vizuri,pia testosterone huathiriwa na hatimaye nguvu za kiume kupungua,kurundikwa kwa mafuta mabaya mwilini na hatimaye kuzeeka haraka. Ndugu msomaji vyakula vya sukari sio vibaya lakini jifunze kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi kuingia mwilini mwako.

KUHUSU TAFITI ZINASEMA NINI KUHUSU ONGEZEKO LA MAGONJWA HAYA SUGU HUKU MAKAMPUNI YAKIZIDI KUTENGEZA DOLLAR ZA KUTOSHA.

Watu wengi ukiongea nao wanakuambia uzito ni wa kurithi. Hii ni kutokujua wanasayansi wamefikia wapi. Miili yenu ina GENES au chembechembe za kurithi kutoka kwa wazazi wetu. Hizi chembe chembe zimo mwilini ili ziweze kusababisha magonjwa hayo zinahitaji kupewa maelekezo au taarifa na haya maelekezo yanatoka katika mazingira hatarishi tunayoishi na vyakula tunavyokula. Hivyo basi hayo maelekezo yanabadili taswira nzuri ya hizo GENES na hatimaye kuanza kusababisha magonjwa kama kuongezeka kwa uzito,pressure,kisukari nk. REMEMBER THAT GENE DOES NOT WORK IN ISOLATED MANNER. THEY RECEIVE INSTRUCTIONS FROM THE ENVIRONMENT AND FOODS WE EAT.
Utafiti uliofanyika katika watu wa mapacha ulionesha kuwa pacha moja alikuwa na kitambi na kisukari. Kumbuka mapacha hawa wana chembechembe za kurithi sawa lakini ilionesha kuwa mmoja ni mgonjwa wa kisukari na uzito kupita kiasi. Uwezekano wa pacha wake kupata kisukari walibaini ni asilimia 13 hadi 30 na hizi asilimia ni kutokana na aina flani ya vyakula walivyoshare walipokuwa bado wanaishi pamoja.
VYAKULA TUNAVYOKULA NA MAZINGIRA TUNAYO ISHI TUNA UPA MWILI MAAELEKEZO YA KUTEKETEZA MWILI. NI DHAHIRI KUWA PESA NA AFYA BORA AFYA LAKINI LEO HII WATU HATUTHAMINI AFYA ZETU KWANI TUNATAFUTA PESA USIKU KUTWA LAIKINI TUNASAHU AFYA ZETU.

NAMNA YA KUCHAGUA VYAKULA VYENYE SUKARI KIDOGO
GLYCEMIC INDEX
Hiki kipimo kinachokadiria wingi wa sukari utakaongezeka baada ya kula aina ya chakula flani.
LOW GLYCEMIC INDEX
Hivi ni aina ya vyakula ambavyo vinaongeza kiasi kidogo cha sukari mwilini. Na hivyo ni vizuri kuhakikisha sukari yako ipo katika hali ya usawa muda wote.

HIGH GLYCEMIC INDEX
Hii ni aina ya vyakula ambavyo vina ongeza kiasi cha sukari kwa wingi mno na ndivyo hatushauriwi kuvitumia ndio chanzo kikubwa cha magonjwa tabia kama uzito kupita kiasi,pressure,kisukari,uvimbe kwenye kizazi,matatizo ya nguvu za kiume na nk. Ndg msomaji ukitaka kujua kuwa tayari umesha anza kuathiriwa na vyakula hivi please zingatia haya,UZITO KUPITA KIASI,WEUSI KWENYE MIKUNJO YA NGOZI ACANTHOSIS NIGRICANS, KICHWA KUUMA OVYO,MACHO KUUMA ,mizunguko mibovu ya hedhi,maumivu wakati wa hedhi nk ni mojawapo ya dalili za mwanzo ya hivi vyakula.

VIFUATAVYO NI VYAKULA NA ALAMA ZAKE ZA KIASI CHA SUKARI KILICHOBEBA
SUKARI YA MEZANI -68
MIKATE MWEUPE-70
MIKATE YA NGANO-70
VIAZI VYEUPE-94
NOTE; GLYCEMIC INDEX VALUE
KAWAIDA 55 AU CHINI YA 55
JUU 70 AU ZAIDI YA SABINI
Jiulize kuna siku inapita hujala hivyo hapo vyakula??? Na je unakula kiwango gani??
SLICE MBILI ZA MIKATE NI SAWA NA SUKALI VIJIKO VIWILI VYA MEZANI…..
VYAKULA VYA MBADALA YA HIVYO HAPO JUU NI HIVI
MKATE MWEUSI AU RYE BREAD
Watu wengi wanshindwa kujua kwa nini tunashauri mikate kama hii ni kwa sababu zifuatazo-
-ZINA NYUZI NYUZI SANA YANI FIBER….Endelea kufuatilia makala zangu umuhimu wa FIBER
-Kiwango kidogo cha sukari- glycemic index 63
-mafuta kidogo
-inaondoa mafuta mabaya mwilini
2. MAGIMBI aka YAM wenzetu watu wa kigoma wanaita MAHOLE. Glycemic index ya 51. Yam zina fiber nyingi na sukari kidogo ndio maana inafaa sana kwako amabaye umeshindwa kupunguza uzito au tayari unasumbuliwa na magonjwa sugu.
3. MATUNDA matunda engi yani glycemic index ya 40-65. Hapa pia kuna matunda ambayo unastahili kula kulingana na uzito na magonjwa tabia mengineyo.
NI DHAHILI KUWA WATU WA NCHI KAMA CHINA,JAPANI NA KOREA NI NCHI AMBAZO SWALA LA UZITO MKUBWA ILIKUWA NI CHANGAMOTO KWANI NI INCHI AMBAZO ZILIKUWA NA MFUMUKO WA VIWANDA. LEO HII NCHI KAMA JAPANI NI NCHI AMBAYO ILIAMUA KUSHUGULIKA NA TATIZO HILI NA HATIMAYE KUELIMISHA JAMII NAMNA YA KULA SALAMA NA HATIMAYE VYAKULA HIVI KULETEWA SISI WAAFRICA WAGUMU WAKUPOKEA MABADILIKO. CHUKUA MFANO MAGONJWA YA KISUKARI,UZITO MKUBWA,FIBROIDS NI MAGONJWA YA WATU WENYE PESA MLALA HOI NI MARA CHACHE SANA KUMKUTA NA HALI KAMA HII.
Kumekuwa na taarifa kuwa kufanya mazoezi unaweza kupunguza uzito. Ahahaha huu ni ushauri unaotolewa na daktari lakini ni dhahiri kuwa kuna watu wanalipia gyme kila siku na hawapungui uzito. Hii ni kutokana kwamba maisha yao hawajabadili kabisa kuanzia mlo,kutopata uzingizi vizuri na mazoezi sasa. Mazoezi hukufanya damu isambae kwenye sehemu mbalimbali ili shuguli za mwili zifanyike ipasavyo pia mazoezi hukufanya kile chakula ulichokula kitumike kufanya kazi. Lakini uwezekano wako kupungua uzito kwa mazoezi ni kazi sana yakupasa kubadili mlo wako mpendwa msopmaji. BADILI MLO WAKO UFIKIE MALENGO YAkO ACHA KUSIKILIZA WATU WANASEMA NINI FUATA USHAURI WA LISHE KUTOKA SEHEMU MAAALUMU.
JE NINI KIFANYIKE KAMA TAYARI UKO ADDICTED NA SUKARI NA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI MWILINI MWAKO?
LIKE PAGE YANGU MAKALA IJAYO NITAZUNGUMZIA ZAIDI NAMANA YA KUPUNGUZA VYAKULA VYA SUKARI NA HUKU LISHE IKIBAKI PALEPALE BILA WEWE KUJINYIMA KULA.

Story By:@Joplus_

Source: Dr. Boaz