Kutana na Edwin Bruno, kijana mwingine wa Tanzania aliyetajwa Forbes

May 28 2016 alianza kutajwa Mrembo Mtanzania ambaye ni Miss Universe Tanzania 2010 Hellen Dause kuwa miongoni mwa Wajasiriamali 30 wa Afrika wenye umri chini ya miaka 30 ambao wanatarajiwa kuwa Mabilionea wa kesho kutokana na kupambana kuzisaka noti kwa kujituma na ubunifu.

Sasa mwingine ni Mtanzania Edwin Bruno ambaye naye yumo kwenye hii list yenye majina kutoka Afrika kwenye nchi kama Zimbabwe, Kenya, Nigeria, Madagascar na Gambia ambapo wanatarajiwa kuwa mabilionea wataotoa ajira kwa maelfu ya watu baadae.

Hellen

 Edwin ni mwanzilishi wa kampuni iitwayo Smart Codes,  ni kampuni inayohusika na kununua matangazo na kuwezesha biashara za kampuni nyingine kuonekana kwenye Mtandao kupitia matangazo hayo ya kwenye Social Media, website n.k kwa bei nafuu na kwa njia iliyosahihi zaidi kwenye teknolojia ya sasa.

Baada ya kutajwa kwenye hii list Edwin anasema ‘Nimefurahia nafasi hii ya kipekee, mimi na timu yangu tumekua tukifanya kazi usiku na mchana kuleta suluhisho kwa Wateja wetu, tumejinyima usingizi kwa muda mrefu kufanikisha na kufikia tulipo

Edwin na kampuni yake mwaka jana walishinda tuzo na ubunifu wao kutambuliwa kimataifa baada ya kubuni APP ya M-PAPER ambayo inamuwezesha mtu kusoma magazeti ya kila siku kupitia mtandao na kulipia nusu bei kuanzia kwenye kurasa za mwanzo, ndani na mwisho kwa kutumia computer au simu ya mkononi.

Source: Millard ayo