KAULI YA ICE CUBE KUHUSU TUHUMA ZA KIFO CHA JERRY HELLER.

Rapa na mwigizaji Ice Cube amejibu tuhuma za kifo cha meneja wa zamani wa kundi lao la NWA Jerry Heller ’75’ kuwa kimesababishwa na alivyoigizwa kwenye filamu ya Straight Outta Compton.

Jerry alifariki September 2 na mwanasheria wake anasema msongo wa mawazo baada ya filamu hio kutoka ulisababisha Jerry kupata matatizo zaidi ya gonjwa la moyo na kufariki kwenye ajali ya Gari huko Thousand Oaks, California.

Jerry alikuwa meneja wa NWA na msanii Eazy-E, Heller alianzisha Ruthless Records mwaka 1987 huko Compton, California, kundi la NWA lilisambaratika 1991, huku Ice Cube, Dr Dre walisema sababu ilikuwa usimamiaji mbovu wa pesa za kundi uliofanywa na meneja Heller.

Ice Cube ameongelea kifo cha meneja huyo nakusema “Taarifa hizi nimezipata nikiwa mtaani na MC Ren na DJ Yella tumetoka mbali wote na meneja Jerry Heller, kifo chake ni sehemu ya maisha, tumezaliwa ili tupite tu na wote tunajua sehemu kubwa ya maisha yetu tuliyokuwa na Heller”

Kabla ya kifo chake Heller alifungua kesi dhidi ya mastaa hawa na watayarishaji wa filamu ya Straight Outta Compton akidai dola milioni $110m kwa kuchafuliwa jina na filamu hio.

Story By :@Joplus_

Source: Sam Misago