Jay Z aachia ngoma ya kwanza.

 

Rapa JAY-Z alipodondosha ujio wa album yake ya 4:44 ambayo mapokezi yake yaliiwezesha kugonga mauzo ya Platnum ndani ya siku chache za wiki, kwa waliofurahia kazi za album hiyo sasa wanaweza kuitazama video ya wimbo wa ‘Kill JAY-Z’ wimbo ambao ni utangulizi wa ngoma 10 zinazokamilisha album.

Ngoma hiyo iliyotayarishwa na producer mkongwe No I.D ambaye alipewa uandaaji mzima wa album hiyo ya 4:44 ikiwa video ya wimbo huo wa utangulizi imeongozwa na Gerard Bush akishirikiana na Christopher Renz.

JAY-Z anategemewa kuachia video ya kazi nyingine soon kwakuwa kwa utangulizi huu ni wazi kuwa mashabiki wakae mkao wa kula pia haitazamiwi kuwa ataishia hapo kulingana na ukubwa wa album hiyo ya 13 katika mfululizo wa album zake.

Source: Dizzim online