Rapa na hitmaker wa ngoma ya ‘Muziki’ anayeendelea kufanya vyema kupitia kazi yake mpya ametimiza idadi ya watamaji zaidi ya milioni moja kupitia video ya wimbo wake wa ‘Hasara roho’ katika mtandao wa Youtube ndani ya muda wa wiki moja pekee.
Wimno huo wa Hasara roho wa Darassa umeonekana kuwa na mapokezi mazuri kiasi cha mashabiki baadhi kutoa maoni huku wakiulinganisha na wimbo wake uliotangulia wa ‘Muziki’. Hasara roho umeonekana kuvunja record ya wimbo wa ‘Muziki’ kutokana na kuushinda kasi ya utazamwaji katika mtandao wa Youtube.
Video ya ngoma ya ‘Muziki’ ilipata watazamaji zaidi ya milioni moja ndani ya wiki mbili jambo ambalo limekuwa tofauti kwa wimbo wa ‘Hasara roho’ kutokana na kuwa video imepata kutazamwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya wiki moja.
Wimbo huo umeandaliwa chini ya watayarishaji watatu ambao ni ABBAH THE PROCESSOR, MR. T TOUCH na Mr. VS upande wa audio huku video hiyo ikiwa imeongozwa na Director wa video za muziki mwenye historia nzuri ya video zake kufanya vizuri ‘Hanscana’ ambaye ameshafanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa Tanzania ambao ni pamoja na Diamond Platnumz katika video ya Nasema nawe, G Nako katika video ya Arosto, Chin Bees katika video ya Pakaza na nyinginezo nyingi na mastaa tajika.
Hata hivyo wimbo huo wa Hasara roho wa Darassa umeonekana mara kadhaa katika mzunguko wa kuchezwa katika vituo vikubwa vya matangazo hasa runinga ikiwa ni pamoja na Trace Tv Africa na dalili nyingi za mashabiki kuonekana mtandaoni katika video fupi fupi wakionekana kufurahia uzuri wa wimbo huo.
Source: Dizzimonline