Joh Makini aitaja Don’t Bother kama ngoma iliyomfungulia njia kimataifa

Kwa haraka haraka inawezekana usione ukubwa wa single kadhaa za Joh Makini hasa nchi za nje lakini kwa sasa inabidi ujue kuwa ‘Don’t Bother’ kwake ni single kubwa na anayoiheshimu kwasababu imemwezesha kutoboa mipaka ambayo mwanzoni ilikuwa ngumu kwake kutoboa.

“Imeniongezea uthamani na imenitambulisha Nje kwa kiwango kikubwa sana. Let’s say mpaka unapata air time kwenye nchi kama South Africa na watu wanakujua kwa kiwango fulani ni kwasababu ya kolabo na AKA,” Joh aliiambia 255 kwenye kipindi cha XXL, Clouds FM.

Aliongeza,”AKA ukiwataja matop 3 wa pale South wanaofanya vizuri kwenye mainsteam huwezi kuacha kumtaja. Kumpata mtu kama AKA ufanye naye kolabo ni kazi kwahiyo unapofanya kazi na mtu kama yule inakutengenezea respect watu wanakuwa wanaheshimu u-serious wako ulionao kwenye kufanya kazi wasichukulie poa.”

“Hatujawahi kuongea naye kuhusiana na kufanya kazi nyingine ya kwake au ya kwangu lakini maybe siku za usoni you never know.”

Hivi karibuni Joh Makini anatarajia kuachia ngoma yake aliyomshirikisha Davido.

Source: Dizzimonline