Staa gani wa Bongofleva kapata mtoto wa kike leo?

Mwaka 2017 umeshuhudia mastaa kadhaa wa Bongo wakifurahia kupata watoto, wengine wakifurahia maisha mapya ya ndoa lakini wengine pia sasa hivi nao wanategemea kupata watoto kabla mwaka haujaisha.

Leo July 25, 2017 staa wa Bongofleva Linah Sanga ambaye alikuwa mjamzito amepata mtoto wa kike ambaye amejifungua salama katika Hospitali ya Marie Stopes, Dar es Salaam.

Taarifa kwenye Instagram ya Mpenzi wa Linah, Director Ghost ambaye kaweka picha yenye maneno ‘It’s a Girl’ na kuandika “Alhamdullilah” imekuwa ikisambaa.

Source: Millard ayo