Diamond platnumz Amrudisha Hawa

NAJARIBU KUITAFAKARI TU KUIVUTIA PICHA YA WIMBO WA NITAREJEA PART2 ITAKAVYOKUWA KALI NA YENYE MSISIMKO.

Wakati @diamondplatnumz yuko kwenye mapenzi moto moto na na mpenzi wake HAWA maisha yalikuwa magumu na ikabidi diamond amuage mpenzi wake kuwa anaenda kutafuta maisha ila akamuahidi kuwa NITAREJEA.Diamond akiamini kuwa mjini atapambana na maisha afanikiwe arudi kwa mpenzi wake hawa alizidisha sana juhudi katika kazi yake na ubunifu mkubwa hasa ukizingatia kazi yake ni ya muziki.Ukweli mungu alimjalia @diamondplatnumz alipambana sana na kipaji chake na akafanikiwa kufikia malengo aliyotataka.Ila katika harakati za kupambana diamond alijikuta kwenye mahusiano na mabinti mbali mbali ambao walimpelekea diamond kumsahau mpenzi wake wa zamani Hawa.Baada ya muda Hawa naye alisubiri kama mpenzi wake diamond atarejea bila mafanikio na ndio hapo na yeye akaamua kuanzisha mahusiano na mwanaume mwingine ambaye walifikia kabisa kufunga ndoa.

Kutokana na kila mtu kuwa na mahusiano yake iliwafanya kabisa kusahauliana na kila mtu kuendelea na maisha yake.Ila ukweli kwa Hawa hali haikuwa nzuri kwa sababu alijikuta katika makundi mbali mbali ambayo yalimfanya kupotea kabisa ki maisha na hata ndoa yake kuvunjika.Wakati diamond akiwa mahusiano yake yako imara ila alipata kukumbuka yale mema aliyofanya na mpenzi wake wa zamani Hawa na kuonesha kutamani japo kujua yuko wapi japo sio wapenzi tena. Ila wakati diamond akiendelea kutamani kujua Hawa yuko wapi ghafla zinazuka habari kuwa sasa hivi Hawa kawa mlevi wa gongo na maisha yake yote yameharibika kitu ambacho kiliwashtua watu wengi pia.

Kuzuka kwa habari hizo tunaaamini zitasaidia kumfikia mpenzi wake wa zamani diamond ambaye alikuwa anatamani siku kujua Hawa yuko wapi kwa mana hiyo diamond atarejea kwa Hawa safari hii japo anarejea kama rafiki ambaye anatamani kumuona mpenzi wake wa zamani Hawa akirudi kama zamani kwenye kipaji chake.

JE UKIPEWA NAFASI YA KUTOA JINA LA WIMBO HUO UTAUPA JINA GANI? .

Source: Udaku