Huwezi nifananaisha na Diamond na Alikiba.

Aslay hataki watu wamfananishe na Diamond na Alikiba, amesema yeye bado hajafikia level hizo ila anajitahidi na yeye afike walipofikia ili aweze kuitangaza nchi yake na muziki wake.

“Sio kitu kizuri kwa upande wangu, kwasababu alikiba kazi yake inaonekana na anafanya vizuri so ukisema unanifananisha nae unakoa sio vizuri, sio alikiba tu msanii yoyote usinifananishe nae ambaye yupo tayari kwenye level nyingine na mimi, siwezi kufanana na Alikiba wala Diamond” Aslat aliiambia Sammisago.

“Siwezi kuwa Top kwa wasanii wa Bongo Fleva, ukinbiita mimi top inakuwa uongo ila nitajitahidi nifikie hatua zile, ila siwezi kuwa top, sio kwasasa hivi” Aslay aliongeza.

Pia alisema yeye kwasasa anajitahidi kuachia ngoma kali tu ili kufikia hatua kubwa ili aweze kuitangaza nchi yake.

Source: Team Tz.