Loveness diva atoa ya moyoni

                                                       

Ni kweli mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho, Diva The Bawse ni mjamzito? Hilo ndio swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza tangu Jumamosi hii kutokana na picha ya Ultra Sound iliyokuwa ikisambaa mitandaoni.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo alikataa kuwa si mjamzito na picha inaonekana mitandaoni ni yake kweli ambayo alienda hospitali kuangalia kama ana uvimbe tumboni kutokana na operesheni aliyofanyiwa mwaka juzi.

“Ile ultra sound ni yangu, nilienda check kama nina uvimbe tumboni maana had surgery ya mwaka juzi nikakuta hamna uvimbe and nikasema it catches my soul maana i was worried, sijaandika Im pregnant,” amesema Diva.

“Siwezi kusema I’m a pregnant, i keep it to myself sababu sio vizuri kutangaza hayo mambo mapema mapema, anything can happen lakini nina uwezo wa kuzaa watoto mwisho wa 5,” ameongeza.

                                                                    Source: Udaku