Mwezi uliopita tulizipata taarifa za mfalme wa muziki wa Taarab Mzee Yusuph kuachana kabisa na biashara ya muziki na kuamua kurudi kumuabudu Mungu kwa imani ya dini yake.
Mengi yalisikika na wengi waliongea lakini jambo hilo limemkuna vilivyo hitmaker wa ngoma ya “Komela” Dayna Nyange na kufunguka kuwa anatamani na yeye angekuwa na imani kama ya Mzee Yusuph.
Akipiga story na Perfect255 Dayna amefunguka kuwa ni vigumu sana mtu kufikia maamuzi ambayo amefikia Mzee Yusuph labda uwe na baraka za Mungu ndani yako.
“Mwenyezi Mungu anampenda sana Mzee Yusuph, kuna maamuzi mengine huwezi kuyafanya kwa hali ya kibinaadam ya kawaida, mpaka uwe na baraka za mwenyezi Mungu, mpaka Mungu akuchague kufanya kile kitu, sio kitu cha kirahisi. Mfano mzuri ni kama mimi sasa hivi hata nisikie sauti inatoka mbinguni inaniambia niache muziki sidhani kama nitaweza.”
Yapo mengi aliyoyazungumza Dayna Nyange na full interview nimekuwekea hapa chini unaweza kuitazama.
Story By:@Joplus_
Source: Perfect255.com