Dayna Nyange Asogea Kimataifa Zaidi.

Mwimbaji staa wa kike kutoka Bongoflevani Dayna Nyange ambaye ni mshindi wa Best Vocal Performance Female na Best African Artiste katika BAE Awards 2017 ambapo tangu hapo hakutoa wimbo mpya.

Sasa good news ni kwamba Dayna alikuwa Afrika Kusini kwa ajili ya kutengeneza video mpya ambapo alikutana na mdogo wake Drake wa Marekani.

Ni video yangu niliyoifanya siku siyo nyingi na ninaiachia leo. Ni video ya tofauti na kubwa kwani wimbo ambao nahisi utanisogeza na kunifikisha hatua kubwa. Nilivyofika South Africa nilipata ugumu kumpata mtu wa kushoot naye nafasi ya mwanaume.

“Nilipata zali  baada ya kumpata mdogo wake Drake ambaye ndiye nimefanya naye video yangu, japo sikuamini nilivyoambiwa.

“Ni mara yangu ya kwanza kufanya video South Afrika na ugumu ulikuwepo maana kila kitu ni kigeni kama ma modal wa kule ni gharama sana na kuna vitu ambavyo vilikuwa vinatakiwa mapema lakini hatukuvifanya ikawa changamoto hivyo tukakuta tumebakiwa saa nne ambapo ndio tukakutana na mdogo wake na Drake.

“Sikuwa nategemea kushoot na mdogo wake Drake na haikuwa rahisi ila marafiki zake wakamshawishi ambapo wakati pia na-shoot sikuwa nategemea nilikuwa na-imagine kama ni kweli kakubali au la. Tuli-shoot video kwa siku tatu na video itakuwa YouTube  Dayna Nyange.

Source: Millard ayo