CHRISTIAN BELLA AWAPA MCHONGO SHABIKI ZAKE KWA KUWEKA MTONYO WA LAKI 1 KWA ATAKAYEWEZA KUFANYA ALIYOYAELEKEZA.

King of the Best Melodies Christian Bella leo ndani ya Perfect255 anatoa Deal exclusive kwako wewe shabiki wake ambaye utaweza kugundua vitu flani flani katika remix ya Ukimwona.

Wewe si shabiki mzuri wa ngoma za Christian Bella, huu mchongo unakuhusu sana, sasa kama utaweza kugundua vitu flani flani hivi katika “Ukimwona Remix” aliyoifanya baada ya  Ukimwona ya Diamond basi huu mchongo lazima ukudondokee.

Akiongea na Perfect255, Bella alifunguka katikati ya mazungumzo yake alipokuwa anaongelea juu ya maswala ya uhalali wa wasanii kurudia ngoma za wasanii wengine waliowahi kufanya vizuri au wanaoendelea kufanya vizuri katika Game ya Bongo fleva ndipo akaamua kutoa fursa hiyo kwa mashabiki wake kugundua vitu ambavyo vinapatikana katika ngoma yake ya “Ukimwona Remix”

Msikilize hapa.

Sasa 255 inasimamia mchongo huu, niandikie mimi kwenye page yangu ni ngoma gani ya Bella inatokana na ukimwona Remix.

Story By:@Joplus_

Source:Perfect255.com