CHRISTIAN BELLA ASISITIZA KUKOSEKANA KWA UMOJA KWA WASANII WA DANCE NDIO CHANZO CHA KUSHINDWA KUFANIKIWA.

Tuki throwback mwezi mmoja nyuma tutagundua kuwa Perfect255 iliwahi kukuletea story ya rapper Staminah akiwatolea mapovu wasanii wenzake ambao walishindwa kusapoti kazi yake ya “Mmeniroga remix” hata kwa kuposti cover kwenye page za mitandao yao ya kijamii.

Sasa time hii ni zamu ya mkali anaefanya muziki wa dance Christian Bella kufunguka kuwa kitu kikubwa kinachofanya wasanii wengine wa dance washindwe kufikia level zake ni kwasababu hawataki kuungana na kuwa kitu kimoja ili wapeane sapoti kama ilivyo kwenye Bongo Fleva.

Akiongea na Perfect255 Christian Bella amedai kwamba wengi wa wanamuziki wa dance wana chuki binafsi na hawapendani wenyewe kwa wenyewe na hiyo ndio sababu kubwa inayo wafelisha na kufanya muziki wao usifike mbali zaidi.

“Siku zote siri kubwa katika maisha ni kutafuta baraka kutoka kwa Mungu. Kuna tabia zingine zinaziba baraka kutoka kwa Mungu,  moja kati ya hizo ni kutomuamini mwenzako ambaye ameshapiga hatua. Wasanii wengi wa bendi hawapendi kukubaliana na ukweli, wana chuki binafsi.”

Christian Bella alitolea mfano kwa wasanii wa Bongo Fleva pale msanii mmoja anapotoa cover ya kazi yake na wengine kutoa sapoti kwa kuisambaza katika page zao za mitandao ya kijamii na kudai kwamba kwenye muziki wa dance huwezi kukiona kitu kama hicho.

Yapo mengi ambayo aliyazungumza Christian Belaa, na yote nimeyakusanya hapa kwenye hii video hapa chini ambayo ina full interview. Itazame ujifunze mengi kutoka kwa Christian Bella.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com