Bodi ya Filamu Tanzania imeeleza sababu za kufungia baadhi ya filamu

Kumekuwa na taarifa za kufungiwa kwa baadhi ya filamu Tanzania kutokana na sababu mbalimbali huku baadhi ya watu wakihoji kuhusiana na kufungiwa kwa baadhi ya filamu hizo.

Joyce Fisoo ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania hapa anaielezea millardayo.com na AyoTV sababu za baadhi ya filamu kutoka Bongo movie kufungiwa.

>>>”Kuna baadhi ya movie zinaletwa hadithi hazina mahusiano na kile kinachowekwa. Kwa mfano, scene nyingi za vitandani, za mapenzi, unakuta hadithi kwa namna yoyote iwayo haijamtaka yule muongozaji kufanya au kuwa na muhusika atakayekuwa kitandani.

“Sisi pale ambapo hadithi itataka uvae nguo fupi tunatambua ujumbe unatakiwa ufike kwa aina ya vazi lakini kama unatuvalia nguo fupi wakati unatuchezea scene ya ofisini ukiwa na nidhamu tutakuuliza” – Joyce Fisoo

                                                              Source: Millard ayo