Legend Producer wa Bongo Bob Manecky amesema kuwa Wanene wamefanya uwekezaji mkubwa lakini uzalishaji wao hauridhishi licha ya kuwa na studio nzuri na vifaa vingi ila wanashindwa kuvitumia.
Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Bob Manecky amesema hata yeye anaitazama studio kuwa anaweza kufanya kazi endapo angeamua kutoka nje ya AIM Records.
“Kwa sasa hivi, nikisema nichague sehemu ya kufanya kazi hata kwa miezi 3, nitachagua Wanene kwa sababu wana vifaa vingi sana ila wanashindwa kuvitumia. Wale wahindi hawajui Bongo Fleva, ila Wanene wana bonge moja la studio Tanzania, lakini hamna hit.
“Sisi tumeanza na studio hata watu watano wakiingia walikuwa hatoshei, lakini tulitengeneza hit song mpaka zikachukua tuzo. Kwa hiyo, ukubwa wa chumba siyo issue, ni akili ya mtu. So, ubunifu hawana. Sio kila mtu anakuwa nao.” – Bob Manecky.
Source: Millard ayo