Alichojibu Harmorapa baada ya Wema Sepetu kumtolea nje ombi lake

Siku kadhaa zilizopita staa wa Bongo Fleva Harmorapa aliweka wazi kumzimia staa wa Bongo movies Wema Sepetu baada ya kudai anaweza kumgharamia kwa kila kitu na baadaye April 5 2017 Wema Sepetu kupitia Instagram alimtaka Harmorapa aache kujinadi na asiiharibu image yake.

Sasa leo baada ya kumfikia ujumbe kutoka kwa Wema Sepetu akionywa kuhusu wazo lake hilo, Harmorapa ameongea na millardayo.com na AyoTV Entertainment alivyoupokea ujumbe huo.

>>”Unajua kwamba hata unapotongoza ama unapoomba kitu kuna mawili; kuna kukubalika na kukataliwa. Kwa hiyo yeye alichokiongea tayari kishaongea. Kwa hiyo haina haja sana kulijadili kwa sababu ameshaongea.” – Harmorapa.

Source: Millard ayo