Cassper Nyovest, Future & Diamond kwenye steji moja Dar es salaam


Rapa Cassper Nyovest kutoka South African atakutana na mastaa Diamond Platnumz kutoka Tanzania na Future kutoka Marekani kwenye stage moja ambapo watafanya show mwezi July mwaka huu. Future na Cassper watakutana kwanza Maputo Zambia na kumaliza Dar es salaam.

Mastaa wengine kutoka Marekani wanaotarajiwa kutua Afrika ni pamoja na Travis Scott na Bryson Tiller ambao watapiga show jijini  Johannesburg na mji wa Polokwane mwezi June mwaka huu.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa rapa Future kufika Tanzania na Zambia, mwaka 2016 Future ambaye jina lake halisi ni Nayvadius DeMun Wilburn alifika Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMAs) na kufanya show yake pamoja na Cassper Nyovest, Diamond Platnumz, Emtee, Kwesta, Patoranking, Ali Kiba, Babes Wodumo, Nasty C, YCee na Yemi Alade.

Source: Millard ayo