Msanii wa muziki na hitmaker wa ngoma ya ‘Muziki’ Darassa ambaye yuko nchini Kenya kwa ajili ya onesho la ‘B-Club Pool Party’ amrzungumzia wimbo uliosikika kipindi ambacho watu walingoja na kudhani ni ujio mpya baada ya kungoja kwa kipindi kirefu.
Akizungumzia ngoma hiyo ambayo baadhi waiopata nafasi ya kuusikiliza waliupatia jina la ‘Utanitoa roho’ Darassa amesema kuwa wimbo ulivuja ukiwa haujaisha kosa ambalo lilitokea kipindi ambacho alikuwa katika mikakati ya kuubadilishia mashairi kwa lengo uboreshaji zaidi.
“kwa bahati mbaya au nzuri nafikiri ni mistake ambayo wenyewe kwenye timu yetu hatujui nani ambaye anahusishwa…tushapatwa na matatizo ya kupoteza flash…huo wimbo kipindi uko demo na tulikuwa na plan ya kubadilisha haya mashairi tukiamini tungeweza kuweka mashairi bora zaidi. So wakati mimi nasikiliza beat chorus wakati natembea kwenye misele yangu tubadilishe haya mashairi tunatumiwa WhatsApp kipande cha huo wimbo kwamba watu wao mtaani wanasikiliza” Alisema Darassa Alipokuwa akihojiwa na Mambo Mseto ya Radio Citizen.
Hata hivyo Darassa hakubainisha kama wimbo huo utafabyiwa marekebisho ili utoke ukimwa kamili na ubora mwingine bali aliwataka mashabiki kuwa tayari kwa ajili ya kazi mpya iliyotajwa kuchiwa wiki ijayo.
Source: Dizzimonline