Rapper mdogo anaefanya poa sana kwenye game ya bongo fleva Young Killer amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwa kuisubiri ngoma ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni, ngoma ambayo anahisi itakuwa ndio ngoma kali kuzidi ngoma zake zote ambazo amewahi kufanya.
Akiongea na E-News ya EATV Young Killer amefunguka kuwa “Wimbo wangu wa Mtafutaji bado unafanya vizuri lakini nawaahidi mashabiki zangu ngoma ntakayokuja kuitoa, naamini ndio ngoma yangu best kuliko ngoma zangu zote ambazo nimewahi kuzitoa”
Young Killer pia alitoa ahadi kwa mashabiki zake kukaa tayari kuipokea video ya wimbo wa Mtafutaji muda wowote kuanzia sasa.
Story By:@Joplus_
Source: Perfect255.com