Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake


Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa.

Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa.

Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum.

Spinachi
Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka.

Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele.

Chai ya Kijani (Green tea)
Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.

Mafuta ya samaki
Zipo aina nyingi za mafuta ya samaki. Lakini mafuta ya samaki wenye asidi ya Omega-3 yana virutubisho ambavyo huongeza kiwango cha ‘dopamine’ kwenye ubongo.

Dopamine ni eneo la ubongo linalofanya kazi ya kudhibiti faraja na hisia.  Kama dopamine itaongezeka basi mwanamke hujisikia kuridhika anapokuwa na mwenza wake.

Chokoleti
Pamoja na utamu wake, lakini ‘chocolate’ ina virutubisho na madini ya magnesium ambayo humfanya mwanamke kuridhika. Pia huufanya ubongo wa mwanamke kutulia kwa kuondoa msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ukiisha ni rahisi kwa mwanamke kupata hamu ya tendo la ndoa.

Source: Udaku