Viongozi Mbalimbali Waisifu Ngoma Ya Alikiba.


Kiongozi Mwingine ambaye aliwahi kuwa waziri wa Nishati na Madini Willium Ngereja naye ameonekana kuguswa na wimbo huo na kuamua kumpongeza Kiba n kuandika Hivi kweenye Ukueasa wake wa Instagram

“King @OfficialAlikiba : Nyimbo ya Seduce me umeitendea haki tasnia ya muziki nchini pia utaitambulisha nchi yetu kimataifa. Hongera”

Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi ameweka hisia zake hadharani kwa kumsifia Alikiba kwa uzuri wa wimbo wake mpya wa ,Seduce me’ huku akiahidi kumpatia zawadi yoyote aipendayo

Mhe. Hapi ameshindwa kuzuia hisia zake juu ya wimbo huo mpya wa Alikiba ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo aachie ngoma hiyo baada ya kukaa mwaka 1 na miezi kadhaa tangu alipotoa wimbo wake wa Aje .

“Nimekuelewa sanaa wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule.Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli.Keep the fire burning!”,ameandika Mhe Ally Hapi.

Wimbo huo ambao tayari umeshavunja rekodi ya kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Tanzania unaonekana kuwavutia mastaa kibao hapa nchini akiwemo Wema Sepetu.

Source: Udaku.