Vanessa Mdee kwenye jengo moja na Drake, Nicki Minaj na wengine

                                     

Mwimbaji wa Bongofleva Vanessa Mdee yupo nchini Marekani ambapo amepata nafasi ya kuwa miongoni mwa Wageni waalikwa waliohudhuria tukio miongoni mwa matukio makubwa ya mwaka, tuzo za Billboard 2017 Las Vegas Nevada.

Tuzo hizi zina utaratibu wake na sio kila mtu anaruhusiwa au anaweza kuingia tena na kupita kwenye Red Capert lakini mwimbaji Vanessa Mdee kutoka Tanzania amepata nafasi hiyo May 21 2017.

Vanessa Mdee ameiambia millardayo.com na AyoTV kwamba alihudhuria utoaji wa tuzo hizi kwa mwaliko wa timu ya Ludacris lakini pia vilevile yuko Marekani kumalizia ngoma yake na Major Lazer, wale wakali wa hits kadhaa ikiwemo ‘lean on’

                       Source: Millard ayo