Dogo Janjaro Anyoosha Roho Kwa Uwoya.


Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja amezungumzia taarifa zilizokuwa zikidai kuwa anatoka kimapenzi na Muigizaji wa filamu Irene Uwoya.

Rapper huyo ambaye ameachia ngoma mpya leo ‘Ngarenaro’ Amesema  kuwa ukaribu wake na uwoya  ulikuwa wa kawaida tu na hakuna kilichokuwa kinaendelea kati yao ingawa watu waliwachukulia vinginevyo.

“Nampenda sana yule dada lakini kuwa na mazoea naye kidogo kumezua maneno mengi,” amesema Dogo Janja.

July mwaka huu zilienea taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameonakana jijini Mwanza katika matanuzi ya nguvu kitu kilichozua minong’ono kuwa wapo mapenzini.

Source: Udaku