Mwanafunzi Aliyenusurika Katika Ajali Arusha Aeleza

KUFELI kwa breki la basi la shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucy Vicent na udereva usio na uzoefu, vinahofiwa kuwa sababu ya ajali ya basi hilo iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa basi hilo.

Akizungumza jana , mmoja kati ya wanafunzi wasiozidi watatu walionusurika kwenye ajali hiyo, Urusula Godfrey, alisema mvua kubwa ilikuwa ikiyesha kabla ya ajali hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa Urusula, ghafla aliona gari limeruka ambapo yeye wanafunzi wenzake wakiwemo waliokufa katika ajali hiyo, walibaini si mruko wa kawaida na mara moja walianza kupiga kelele za kuomba msaada.

Wakati wakipiga kelele hizo bila msaada, Urusula alisema alishuudia basi hilo likianza kuserereka mpaka mtoni (Mto Marera), ambako lilipinduka na kuanza kuviringika.

Baada ya hapo Urusula alisema hakutambua kilichoendelea zaidi ya kujikuta tu yupo hospitalini, alisema na kushindwa kuendelea kusimulia mkasa huo na kuanza kububujikwa na machozi kwa uchungu.

Source: Udaku