Wanavyopita Wenye Kuhitaji Msaada

Ni karaha kukwepa njia wanayopita maskini na ni sunnah kutokezea mbele ya waombaji na kuwasaidia kitoshelevu kwa kutoa sadaka.

Muhammad bin Yaqub Kulayni amenakili riwaya kutoka Abu Nasar kuwa yeye amesoma barua ambayo Al Imam ‘Ali an-Naqi a.s. alimwandikia Abu Ja’afar (Mutawakikl, mtawala wa Ki-Abbasi). Humo kulikuwa kumeandikwa:
“Ewe Abu Ja’afar! nimepata habari kuwa wewe unapotoka nje wakati umekaa juu ya usafiri wako basi wafanyakazi wako wanakutoa nje kwa kupitia mlango mdogo, ili kwamba yule ambaye ana shida na mwenye kuuhitaji msaada wako asiweze kufaidika hivyo.

Mimi kwa kiapo cha haki yangu ninakusihi kuwa kutoka kwako na kuingia kwako uwe kupitia mlango mkubwa na uwe na wingi wa dhahabu, fedha na mali ili atakapo tokezea mbele yako mwombaji mwenye shida uweze kumsaidia. Wajomba zako wanapokuomba uwape Dinar hamsini na wake zao wanapokuomba uwape Dinar ishirini na tano na usiwape chini ya hapo kama utawapa zaidi basi hilo ni shauri lako.

Na hii nakuambia kwa sababu iwapo wewe utafuata hivyo basi Allah swt atakuwia wema, hivyo utumie na usiwe na shaka katika ahadi na neema za Allah swt mmiliki wa malimwengu yote.”

story@moodyhamza