Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amefunguka kwa kumpa pole mwanadada Vanessa Mdee ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutumia na kusambaza dawa za kulevya.
Nay wa Mitego ameonesha kuguswa na tukio hilo lililomkuta Vee Money ambaye azimepita siku tano tangu ajisalimishe kituo cha Polisi. Kupitia Instagram Nay ameandika
“Vanessamdee Sijui ulipo anzia, but mpaka apa ulipofikia umepambana sana. Nina imani mungu ndo aliye kufanyia wepesi mpaka kua #BrandKubwa na kupata hatua Ulizo nazo. Naamini Mungu Huyu Huyu ndiye atakae kufanyia Wepesi Kwenye yanayo kukabili ivi sasa. Amini izi ni Changa moto tu na ni Mapito ambayo Binadamu tunapitia kwenye Safari ya kuelekea kutimiza Ndoto zetu,I pray for you my friend Vanessa, naamini brand yako haiwezi haribika kirahisi kwa sababu umepambana sana ni wasichana wachache wenye kuweza ku-fight kama wewe. Mungu ata kusimamia uzidi kusonga mbele, Haya yata pita nina imani utakua strongZaidi. #CashMadame KeepItUp. Napenda kuona Wasichana wakifanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii #VannesaTheBrand wewe ni mwanamke wa shoka. Usiyumbishwe kuwa Mfano. Najivunia uwepo wako kwenye Game”
SOURCE BY: TEENTZ