Matokeo Yanga VS TP MAzembe : Yanga yachapwa 1 – 0 …
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga imecheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya TP Mazembe ya Congo DRC na kukubali kichapo cha goli 1 – 0 .
Yanga ambayo ilifanya maandalizi kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuweka kambi Uturuki na kuwaruhusu mashabiki wa soka nchini kutizama mchezo huo bure katika uwanja wa Taifa, ilianza mchezo huo dhidi ya TP Mazembe kwa kasi lakini ilishindwa kutumia vyema nafasi zilizotengenezwa.
story@moodyhamza