Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Diego Costa arudi Uhispania

Chelsea imekubaliana na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Diego Costa arudi Uhispania.

Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye aliondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.

Raia huyo wa Uhispania hajaichezea Chelsea msimu huu na alitumia wakati mwingi wa mwezi Agosti akiwa Brazil.

Hawezi kusajiliwa kama mchezaji wa Atletico hadi mwezi Januari, wakati ambapo marufuku ya uhamisho iliowekewa klabu hiyo itakamilika.

Timu hizo mbili zitakabiliana Jumatano ijayo katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Costa ambaye ni mzaliwa wa Brazil alijiunga na Chelsea kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha £32m miaka mitatu iliopita.

Alifunga mabao 58 katika mechi 120 za Chelsea ikiwemo mechi 10 za ligi ya Uingereza msimu uliopita ambapo Chelsea ilibuka mshindi.

story@moodyhamza